Biashara Zangu: daftari la biashara kwenye simu yako
Rekodi mauzo ya duka lako, jua stoo iliyobaki, fuatilia madeni ya wateja, toa risiti na uone faida ya kila siku. Ni bure, ni kwa Kiswahili, na inafanya kazi hata bila mtandao.
Mauzo
Rekodi mauzo kwa sekunde, scan barcode kwa kamera, pokea malipo kwa Taslimu, M-Pesa, Mixx by Yas, Airtel Money, HaloPesa, benki au mkopo, na tuma risiti kwa WhatsApp.
Stoo na bidhaa
Jua idadi ya kila bidhaa kwenye kila duka kwa pcs, kg, lita, boksi au katoni, pata onyo bidhaa zikikaribia kuisha, na hamisha stoo kati ya maduka.
Madeni, matumizi na ripoti
Fuatilia nani anakudai, rekodi matumizi ya biashara na upate ripoti za mauzo, faida na bidhaa zinazouzika zaidi kwa Excel au PDF.
Maduka mengi na wafanyakazi
Simamia matawi mengi kwenye akaunti moja na ongeza wauzaji, kila mmoja na duka lake na ruhusa zake.
Pakua Biashara Zangu kwenye Google Play · Faragha · info@biasharazangu.com
Washa JavaScript ili kutumia mfumo kwenye kivinjari hiki.